Idara ya Kukabiliana na Moto na Majanga nchini Japani ilisema theluji nyingi na baridi kali tangu Januari 20 vilisababisha vifo vya watu 30.

Kufikia saa kumi na mbili asubuhi Februari 3, watu 12 walifariki katika mkoa wa Niigata, sita huko Akita, wanne huko Aomori, watatu huko Hokkaido na wawili huko Yamagata. Kifo kimoja kwa kila eneo kimeripotiwa katika mikoa ya Iwate, Nagano, na Shimane.

Jumla ya watu 324 wamejeruhiwa, baadhi wakiwa mahututi, kote nchini humo.

Ofisi ya Baraza la Mawaziri ilisema inachunguza vifo vingine tisa kuhusu iwapo vinahusiana na theluji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *