KUTOKA ANGOLA: “Wenyeji wetu Petro wamefanya maandalizi yote yanayohitajika kikanuni”
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally anasema safari yao ya kwenda Luanda Angola, haikuwa na changamoto yoyote na kuongeza kuwa wenyeji wao Petro Atletico wametekeleza majukumu yao ya kikanuni.
Simba itashuka dimbani Februari 7, 2026 saa 1:00 usiku na mchezo utakuwa LIVE #AzamSports2HD
#CAFCL #Simba