Idara ya Kukabiliana na Moto na Majanga ya Japani imesema theluji nyingi na baridi kali tangu Januari 20 imesababisha vifo vya watu 38 nchini humo.

Kufikia saa 2:30 asubuhi, Februari 5, vifo 14 viliripotiwa katika mkoa wa Niigata, saba huko Akita, vitano huko Yamagata, na vinne katika kila mkoa huko Hokkaido na Aomori.

Jumla ya watu 413 wamejeruhiwa, baadhi wakiwa mahututi, kote nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *