Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi huko Cairo siku ya Jumatano, Februari 4, wakisaini mikataba 18 mipya ya ushirikiano wakati wa ziara yake rasmi ya nne nchini Misri. Uhusiano kati ya Misri na Uturuki umeimarika sana katika miaka ya hivi karibuni baada ya karibu muongo mmoja wa kutengana kidiplomasia, huku maslahi yao sasa yakikusanyika katika maeneo kadhaa ya kikanda, hasa Sudan na Ukanda wa Gaza.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili “walibainiha hitaji la kufikia makubaliano ya amani ya kibinadamu yanayopelekea kusitisha mapigano” nchini Sudan na “kuhifadhi taasisi za serikali,” Rais wa Misri al-Sisi alisema katika hotuba ya pamoja na mwenzake wa Uturuki.

Katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni ya Misri, mkuu wa nchi pia alisisitiza “umuhimu wa kuhifadhi umoja na uhuru wa Somalia na kukataa jaribio lolote la kuigawanya.” Cairo na Ankara ziliunga mkono serikali ya Mogadishu na kulaani utambuzi wa Israel wa eneo linalotaka kujitenga la Somaliland.

Tangu mkutano wa kwanza wa viongozi hao wawili mwaka wa 2024, mikataba zaidi ya kumi na miwili ya ushirikiano ilisainiwa, hasa katika nyanja za kiuchumi, usalama, na ulinzi. Siku ya Jumatano, mikataba 18 mipya ilisainiwa kati ya nchi hizo mbili.

Mkutano kuhusu migogoro ya kikanda

Kwa pamoja, waliunda nusu ya kambi ya nchi zilizofanya mazungumzo kwa ajili ya makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano yanayoendelea Gaza, na kujikuta upande mmoja katika vita vya Sudan, wakionyesha misimamo inayozidi kubadilika katika masuala muhimu ya kikanda. Kulingana na wachambuzi, miunganiko hii ni sehemu ya kuibuka kwa mhimili wa usalama wa kikanda ambao pia unajumuisha Saudi Arabia.

Siku ya Jumanne, Februari 2, rais wa Uturuki pia alizuru Riyadh, mpinzani mwingine wa zamani wa kikanda ambaye Ankara imerekebisha uhusiano naye katika miaka ya hivi karibuni. Ziara hii ya kidiplomasia inakuja wakati ambapo mvutano uliongezeka katika eneo hilo, kabla ya mazungumzo yanayowezekana kati ya Marekani na Iran, ambayo awali yalipangwa kufayika nchini Uturuki kabla ya Tehran kuomba kuhamishiwa nchini Oman.

Ushirikiano wa kijeshi

Uhusiano kati ya Ankara na Cairo ulivunjika ghafla mwaka wa 2013, kufuatia jeshi la Misri kumtimua rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa kidemokrasia, Mohamed Morsi, mshirika wa Uturuki na mwanachama wa Muslim Brotherhood, vuguvugu ambalo tangu wakati huo lilipigwa marufuku nchini Misri. Wakati huo, Recep Tayyip Erdogan alisema kwamba hangewahi kuzungumza au kuketi pamoja na kiongozi wa mapinduzi, Abdel Fattah Al Sisi.

Mnamo mwaka 2024, Uturuki ilikubali kuipa Misri ndege zisizo na rubani za kisasa, kabla ya nchi hizo mbili kutangaza mradi wa pamoja wa uzalishaji wa ndege zisizo na rubani mwaka uliofuata.

Jeshi la Sudan, likiungwa mkono na Cairo na Ankara katika vita vyake dhidi ya wanamgambo  wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), limetumia ndege zisizo na rubani za Bayraktar zilizotengenezwa nchini Uturuki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *