
Mazungumzo haya ndiyo ya hivi karibuni kufanyika baina ya mataifa hayo mawili tangu Israel ilipoanzisha vita vya siku 12 nchini Iran mnamo mwezi Juni na hivi majuzi jamhuri hiyo ya Kiislamu kuanza kuwakamata na kuwashambulia raia wake kufuatia maandamano ya nchi nzima ya kuipinga serikali.
Kwa miongo kadhaa Iran imekuwa ikisisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani, lakini maafisa wake wamekuwa wakitishia kuwa watatengeneza silaha za nyuklia.
Kwa sasa Iran inarutubisha madini ya urani kwa kiwango cha asilimia 60, ambacho ni kiwango cha zana za nyuklia.
Mashirika ya ujasusi ya Marekani yanasema kuwa Iran bado haijaanza mpango wa silaha za nyuklia, ila imefanya matukio ambayo yanaiweka katika nafasi ya kutengeneza silaha za nyuklia, iwapo itaamua kufanya hivyo.