Mwishoni mwaka jana, Iran ilikumbwa na maandamano makali zaidi huku wananchi wakipinga gharama za maisha. Mji mkuu,Tehran, ulifurika mamia kwa maelfu ya waandamanaji wakipaza sauti dhidi ya kushuka kwa thamani ya sarafu yao na kupanda kwa bidhaa muhimu na za msingi katika maisha.
Ghafla maandamano hayo yakageuka kutoka kuwa ghadhabu kwa hali mbaya ya uchumi na kuwa upinzani dhidi ya serikali, waandamanaji wakiwazomea watawala na viongozi wa dini.
Mwanamitindo huyu wa Iran anasema maandamano ya wakati huu yana mchanganyiko wa waandamanaji kuliko yale ya miaka minne iliyopita. Watoto kwa watu wazima, maskini kwa matajiri wote kwa pamoja walikuwa katika maandamano hayo. Hali ilionekana kutulia, yenye matumaini lakini yenye nguvu zaidi. Amesema hata hivyo kwamba ngazi za usalama safari hii zilikuwa kali na zilitumia nguvu kuliko katika maandamano ya miaka minne iliyopita.
Watetezi wa haki za binadamu wanakadiria watu 6,000 wengi wao wakiwa ni waandamanaji waliuawa katika kile ambacho kilitajwa kama msako mkali na wa hatari kuwahi kutokea tangu kuundwa kwa jamhuri ya kiislamu ya Iran mwaka 1979. Sasa wana wasiwasi kwamba huenda idadi hiyo ikaendelea kupanda kutokana na taarifa za mauaji zaidi kuendelea kupatikana.
Shirika la habari la associated Press lilizungumza na raia 6 wa Iran kwa kutuia mfumo wa siri wa mawasiliano, na maji yao yaliendelea kufichwa kutoka na wimbi linaloendelea la kuwakamata waandamani na watu wengine wanaoshukiwa kuunga mkono maandamano hayo.
Wanne miongoni mwa mashuhuda wa mkasa huu walikabiliwa na tuhuma za kukwepa kuzimwa kwa mtandao, huku wawili wakizungumza wakiwa nje ya Iran. Walisema kulikuwa na hisia ya nadra na ukosefu wa matumaini miongoni mwa waandamanaji, ambayo piailikuwa na hofu na mshangao kutokana na kiwango cha ukatili.”
“Nilipotoka nje, siwezi kusema kuwa sikuwa na msongo wa mawazo, hapana lakini sikuwa na njia ya kubaki nyumbani,” alisema mbunifu huyo. “Nilihisi kuwa kama ningebaki nyumbani au kama mtu yeyote angebaki nyumbani kwa hofu, hakuna kitu ambacho kingefanyika.”
“Takwimu hizi haziakisi Wairani wote au idadi ya watu wa nchi hii zaidi ya milioni 85, wenye asili na dini mbalimbali. Hata hivyo, zinatoa taswira ya kipekee ya maisha nchini Iran katika kipindi kigumu”
Iran imekabiliwa na shinikizo la usalama na linalozidi kuongezeka hadi sasa. Iran ilishambuliwa na ndege za kivita za Israeli na Marekani wakati wa vita vya siku 12 mwezi Juni mwaka jana na bado ipo chini ya vikwazo vinavyoongozwa na nchi za Magharibi ambavyo vimeifanya hali ya uchumi wa nchi hiyo kuendelea kuwa mbaya. Wadadisi wanasema kuwa serikali inaonekana kutojali hali ya waandamanaji na wananchi kwa ujumla na badara yake kuingilia maisha yao binafsi huku wao wakiendelea haki na heshima yao.