Klabu ya Simba imetoa onyo kali kwa watu waliotumia nembo za wadhamini wake bila ruhusa katika mkutano binafsi ambao haukutambuliwa rasmi na klabu. Uongozi wa Simba umeeleza kusikitishwa na hatua hiyo, hasa baada ya baadhi ya wahusika kutoa kauli za kashfa dhidi ya Mwekezaji wa Klabu, Mohamed G. Dewji.
Aidha, Simba SC imeiandikia Jeshi la Polisi ili lichukue hatua za kisheria dhidi ya waliohusika, huku ikisisitiza kuwa haitavumilia matumizi yoyote yasiyo halali ya nembo au alama za klabu.