Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka, hundi ya Sh200 bilioni ambazo ni ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu katika siku 100 za uongozi wake
Fedha hizo ni maalum kwa ajili ya mitaji ya kuwawezesha vijana na wanawake.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Alhamisi Januari 5, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Hafla hiyo imehudhuriwa pia viongozi mbalimbali akiwamo Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi.