Hatua hiyo imesababisha hofu ya ushindani mpya wa silaha ulimwenguni. Trump ameyatoa matamshi hayo saa chache baada ya mkataba huo wa New START kumalizika baada ya kudumu kwa miongo miwili.

Trump amesema Mkataba wa New START ulijadiliwa vibaya na umekiukwa kwa kiasi kikubwa. Trump ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba wanapaswa kuwa na wataalamu wao wa nyuklia wakifanya kati kwenye mkataba mpya ambao umeboreshwa na wa kisasa na unaoweza kudumu kwa muda mrefu katika siku zijazo.

Serikali ya Trump mara kwa mara imekuwa ikishinikiza kuwa mkataba wowote mpya unapaswa kuijumuisha China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *