Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali maamuzi mtawalia yaliyopasishwa na baraza la mawaziri la Israel jana Jumapili. Hamas imeyataja maamuzii hayo kuwa ni sehemu ya mradi wa kifashishti, wa kikoloni na wa kilowezi wenye lengo la kulitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina.

Hamas, imesema katika taarifa yake rasmi ya jana kwamba hatua kama  kunyakua ardhi, usajili wa mali za walowezi wa Kizayuni, na kuzinyima kibali manispaa za Palestina zinalenga kusimikaa mamlaka bandiai ya utawala huo, na kufanya maangamizi ya kizazi ya  Wapalestina katika ardhi yao.

Ripoti iliyochapishwa jana na gazeti la mtandaoni la The Cradle imeeleza kuwa baraza la mawaziri la Israel limepasisha hatua kadhaa zilizoratibiwa ili kuharakisha upanuzi wa makaazi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwakwa mabavu na Israel na kushadidisha udhibiti wa eneo hilo. 

Gazeti hilo limeongeza kuwa hatua hizo zimeungwa mkono na mawaziri wawili mashuhuri wa baraza la mawaziri la Israel, ambao ni waziri wa fedha Bezalel Smotrich na waziri wa vita wa utawala huo Israel Katz.

Wawili hao wanajulikana kwa chuki yao kubwa dhidi ya Wapalestina na juhudi zao za kuendelea kudhoofisha haki za watu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Harakati hiyo ya mapambno ya ukombozi ya Palestina imetoa wito wa kuwepo umoja wa kitaifa na muqawama dhidi ya mipango hiyo haramu na kuwataka Wapalestina kukabiliana na utawala ghasibu wa kifashisti na walowezi wake kwa njia zote zinazowezekana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *