Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 1
Cristiano Ronaldo anatarajiwa kusitisha mgomo wake katika klabu ya Al-Nassr na kucheza tena katika klabu hiyo ya Saudi Pro League siku ya Jumamosi.
Fowadi huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 41 amekosa mechi mbili kwa sababu hakufurahishwa na jinsi klabu hiyo inavyoendeshwa. (Sky Sports)
Hatma ya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashford Barcelona inategemea uchaguzi wa rais wa klabu hiyo mwezi ujao.
Mkataba wa pauni milioni 26 kwa mshambuliaji huyo wa Manchester United kwa mkopo, 28, ndio kiini cha ombi la Joan Laporta kuchaguliwa tena. (Times – Subscription Required}
Manchester United itamlenga mshambuliaji wa Everton na Senegal Iliman Ndiaye, 25, ikiwa Rashford atahamia Barcelona kwa mkataba wa kudumu. (Caught Offside),
Bournemouth inapanga kumpa mshambuliaji wa Ufaransa Eli Junior Kroupi, 19, kandarasi mpya yenye unono mwingi kwa nia ya kuzuia kutakiwa na baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya, vikiwemo Chelsea, Liverpool, Real Madrid na Paris St-Germain. (Sun),
Manchester City wanajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 100 kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Nottingham Forest Muingereza Elliot Anderson, 23. (Teamtalks)