PARIS, UFARANSA ToniTerry, mke wa nyota na nahodha wa zamani wa kimataifa wa Chelsea na England, John Terry amekuwa gumzo jijini Paris baada ya kuonekana mtaani akiwa matembezini na mumewe huku ametinga viwalo wa aina yake.

John na Toni Terry walionekana kuwa na furaha zaidi kuliko wakati mwingine wowote, huku Toni akijitokeza akiwa amevalia gauni la uwazi wakati wa matembezi yao ya kimapenzi katika Hoteli ya Ritz mjini Paris juzi Jumamosi.

Nguli huyo wa soka mwenye umri wa miaka 45 na mkewe (WAG) mwenye umri wa miaka 44 walionekana kupendeza sana kwa matembezi hayo, huku John akiwa amevalia suti ya rangi ya bluu na sweta ya shingo ndefu.

TO 01

Kwa upande mwingine, Toni alivutia macho ya wengi alipovaa gauni la kijani la uwazi lenye sketi ya hariri iliyokatwa kwa mtindo usio wa kawaida (asymmetrical).

Aliongeza urefu wake wa kuvutia kwa kuvaa viatu vya visigino vya dhahabu na kubeba begi la rangi ya metali kwa ajili ya mali zake.

Wazazi hao wa mapacha Georgie na Summer walionekana kuachilia msongo wa mawazo kwa wikendi hiyo, baada ya kusafiri hadi mji mkuu wa Ufaransa mapema siku hiyo.

John na Toni walifunga ndoa mwezi Juni 2007 katika Jumba la Blenheim, Woodstock, Oxfordshire, kwenye sherehe iliyodaiwa kugharimu karibu pauni milioni moja (£1m).

John (45) na Toni (44) walionekana wenye furaha isiyo kifani huku Toni akijitokeza akiwa amevalia gauni la uwazi kwa ajili ya usiku wao wa matembezi katika Hoteli ya Ritz, Paris.

TO 02

Miongoni mwa wageni wa harusi yao walikuwapo wanasoka Michael Owen, Ashley Cole, Joe Cole na Jamie Redknapp pamoja na aliyekuwa mke wake Louise, huku Lionel Richie akitumbuiza.

Mwaka 2024, wanandoa hao waliwazawadia mapacha wao magari yanayofanana ya Mercedes kwa maadhimisho ya miaka yao 17 ya kuzaliwa, sambamba na kushiriki video ya zamani ikionyesha watoto hao wakiendesha magari walipokuwa wadogo.

Magari hayo yalionekana kuwa Mercedes A-Class AMG Line Premium Plus, ambayo hugharimu takriban pauni 41,000 (£41,000) yakiwa mapya kabisa.

Daily Mail ilifichua John alipata karibu pauni milioni tano (£5m) baada ya kuuza viwanja ambavyo alikuwa amepanga kujenga majumba mawili ya kifahari.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England alinunua mali hiyo yenye thamani ya pauni milioni 4.5 (£4.5m) miaka kadhaa iliyopita.

TO 03

Baadaye aliibomoa ili kujenga nyumba moja yenye vyumba sita vya kulala na nyingine yenye vyumba vitano, baada ya kupata kibali cha ujenzi.

Kiwanja hicho cha Oxshott ni sehemu ya Crown Estate, mojawapo ya maeneo ya makazi ya kifahari zaidi nchini humo.

Terry amekuwa akijihusisha na maendeleo ya nyumba za kifahari kwa miaka kadhaa na amejenga jalada kubwa la mali za thamani.

Nyumba zote mbili zitakuwa na jiko lenye sehemu ya kulia chakula, chumba cha familia, sebule ya mapokezi, chumba cha kulia chakula, vyumba vya kubadilishia nguo na sebule ya mapumziko. Nyumba yenye vyumba sita pia itakuwa na ukumbi wa mazoezi (gym).

Nyaraka za Ofisi ya Usajili wa Ardhi zilizopatikana na Daily Mail zinaonyesha kuwa kiwanja kimoja kiliuzwa kwa pauni milioni 2.75 (£2.75m).

Kwa upande mwingine, kiwanja kingine kinaaminika kuuzwa kwa kiasi kikubwa cha pauni milioni 2.15 (£2.15m).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *