Mahakama Kuu ya Uingereza imetoa pigo kubwa la kisheria kwa jitihada za serikali ya nchi hiyo za kunyamazisha uungaji mkono wa wazi watu kwa Palestina, baada ya kutoa uamuzi kwamba hatua ya Wizara Mambo ya Ndani wa 2025 ya kupiga marufuku kundi la linalounga mkono Palestina la Palestine Action kwa madai kwamba ni shirika la kigaidi, ulikuwa kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo muhimu, iliyotolewa jana Ijumaa jijini London, inawatetea wakosoaji walioonya kwamba marufuku hiyo ilikuwa ukiukaji mkubwa wa uhuru wa msingi wa raia na utumiaji mbaya na hatari wa sheria za kupambana na ugaidi.

Kundi la Palestine Action, lililoanzishwa mwaka wa 2020 ili kupinga uungaji mkono wa serikali ya Uingereza kwa uvamizi wa kijeshi wa Israel na uhusiano wa makampuni ya nchi hiyo na utawala huo ghasibu, liliwekwa kwenye orodha ya makundi yenye misimamo mikali ya Uingereza mnamo Julai 2025 chini ya Sheria ya Ugaidi ya 2000.

Sifa hiyo iliiunganisha Palestine Action na mashirika ya kigaidi yaliyopigwa marufuku kimataifa, na kufanya kuwa kosa la jinai kuwa mwanachama au kuonyesha uungaji mkono hadharani kwa kundi hilo linalotetea haki za watu wa Palestina-, adhabu yake ikiwa kifungo cha hadi miaka 14 jela.

Waungaji mkono na watetezi wa uhuru wa kiraia walikasirishwa sana na uamuzi huo, wakisema kwamba marufuku hiyo imekataza maandamano ya amani na kuonyesha mshikamano wa watu na Wapalestina badala ya tishio lolote la kweli kwa usalama wa umma.

Katika uamuzi wake, Jaji Dame Victoria Sharp na majaji wenzake wa Mahakama Kuu ya Uingereza wamegundua kuwa marufuku ya serikali haikuwa na uhalali unaofaa na iliingilia kwa kiasi kikubwa haki za uhuru wa kujieleza na kukusanyika.

Uamuzi huo umepongezwa na wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu ukitajwa kuwa ni “ushindi mkubwa” kwa uhuru wa kidemokrasia nchini Uingereza na mapambano mapana ya kupigania haki kwa ajili ya watu wa Palestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *