.

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais Donald
Trump amesema dunia itajua “ndani ya siku 10 zijazo” kama Marekani
itafikia makubaliano na Iran au kuchukua hatua za kijeshi.

Katika
mkutano wa uzinduzi wa Bodi yake ya Amani huko Washington DC, Trump alisema
kuhusu mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu juu ya mpango wake wa nyuklia: “Lazima tufikie makubaliano yenye tija vinginevyo mambo mabaya yatatokea.”

Katika siku
za hivi karibuni, Marekani imeongeza vikosi vya kijeshi Mashariki ya Kati, huku
hatua ikisemekana kupigwa katika mazungumzo kati ya wapatanishi wa Marekani na
Iran nchini Uswisi.

Wabunge wa
chama cha Democrat, na baadhi ya Warepublican, wamepinga hatua yoyote ya
kijeshi kuchukuliwa nchini Iran bila idhini ya bunge.

Katika
maelezo yake, Trump alibainisha kuwa Wajumbe Maalum Steve Witkoff na Jared
Kushner, ambaye pia ni mkwe wa Trump, walikuwa na “mikutano yenye tija sana”
na Iran.

“Imedhihirika,
kwa miaka mingi kuwa si rahisi kufanya makubaliano yenye maana na Iran,”
alisema. “Vinginevyo, mambo mabaya yatatokea.”

Siku moja kabla,
Waziri wa habari wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt alionya kwamba Iran itafanya
la “busara sana” kufikia makubaliano na Marekani, akiongeza kwamba
Trump bado alikuwa na matumaini ya suluhisho la kidiplomasia kuhusu mpango wa
nyuklia wa Tehran.

Makombora na
ndege za ivita za Marekani zilishambulia vituo vitatu vya nyuklia vya Iran mnamo
mwezi Juni mwaka jana, na Ikulu ya White House iliripotiwa kujadili chaguzi
mpya za mashambulizi wiki hii.

Vikosi vya
Marekani vimekuwa vikiongeza uwepo wao katika eneo hilo katika wiki za hivi
karibuni, ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwa meli ya kivita ya USS Abraham
Lincoln.

Picha za
setilaiti pia zimeonyesha Iran ikiimarisha vifaa vya kijeshi, na Kiongozi Mkuu
wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamanei, amechapisha ujumbe kwenye mitandao ya
kijamii akitishia vikosi vya Marekani.

“Rais
wa Marekani husema kila mara kwamba Marekani imetuma meli ya kivita kuelekea
Iran. Bila shaka, meli ya kivita ni kifaa hatari cha kijeshi,” moja ya ujumbe
wa Khamenei ulisema.

Wabunge
kadhaa wa Bunge la Marekani wameonyesha kupinga hatua yoyote ya kijeshi dhidi
ya Iran.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *