• Familia moja inatafuta majibu kufuatia kifo cha ndugu yao ambaye alifariki katika mazingira yasiyoeleweka
  • Familia ya Consolata Nduku ilionyesha kutoridhishwa na taarifa za kifo chake, kinyume na maelezo yaliyotolewa na uongozi wa shule
  • Shule hiyo ya Machakos ilidai kwamba walijitahidi kuokoa maisha yake, lakini kwa bahati mbaya, mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu alifariki

Familia moja iliyojaa huzuni katika kaunti ya Machakos imetumbukia katika majonzi kufuatia kifo cha kutatanisha na kisichotarajiwa cha mpendwa wao.

consolata
Faith Ndunge (kushoto) akimlilia mjukuu wake Consolate Nduku (kulia). Picha: Citizen TV Kenya.
Source: Youtube

Marehemu aliyefahamika kwa jina la Consolata Nduku, inadaiwa aliugua akiwa katika shule ya bweni na baadaye kufariki dunia.

Kulingana na familia yake, wasimamizi wa shule ya upili ya Katoloni waliwafahamisha kuwa jamaa yao alikuwa mgonjwa na alikuwa akikimbizwa katika hospitali ya Machakos Level 5.

Hawakujua kuwa muda sio mrefu wangepokea taarifa hizo mbaya kuwa binti yao wa kidato cha tatu hayupo tena.

“Niliwauliza jamaa zangu kama wamepata gari, wakasema wamepata. Tulikutana kando ya barabara na tukasafiri pamoja. Tulipofika tulikokwenda, msichana wangu hakuwepo tena. Alikuwa tayari amekufa,” bibi yake Nduku, Faith Ndunge, alisema kwa machozi.

Pia soma

Karen Nyamu Aonekana Kukasirika baada ya Kusukumwa na Umati wa Watu kwenye Video Iliyopepea

Subscribe to watch new videos

Mjomba wa Consolate Nduku azungumza kwa uchungu

Kifo cha Nduku kiliiacha familia yake ikiwa imechanganyikiwa, huku kukiwa na maswali mengi kuliko majibu, walipokuwa wakitafuta ufafanuzi wa kile kilichotokea kabla ya kutangazwa kuwa amefariki alipofikishwa hospitalini.

Ndunge alisema kuwa mjukuu wake hakuwa na hali yoyote ya kiafya inayofahamika, jambo lililofanya kifo chake cha ghafla kuwa cha kutatanisha zaidi.

“Huyu ni mtu ambaye hakuwa na matatizo yoyote ya msingi, na sasa hayupo tena. Hakuwahi kusema kuwa anaumwa. Mara tu tulipopewa taarifa ni pale shule ilipopiga simu na kusema kuwa alikuwa mgonjwa, na dakika iliyofuata Nduku alikuwa amefariki. Tunauliza maswali mengi,” Ndunge aliongeza.

Mjombake Nduku, Alphonse Muli, alisimulia visa vya awali ambapo wazazi waliarifiwa kuhusu vifo vya watoto wao chini ya hali isiyoeleweka

Mkuu wa Shule ya Katoloni Senior azungumza

Alidai kuwa ni makosa kwa wazazi kutojuzwa mara kwa mara kuhusu ustawi wa watoto wao shuleni, ila kuitwa tu kuchukua miili yao.

Pia soma

Video ya Njugush Akilalamikia Kuteseka Katika Ndoa Yaibuka Tetesi za Kutengana na Wakavinye Zikienea

Uongozi wa shule ulikanusha madai ya uzembe au ucheleweshaji wa kuarifu familia kuhusu hali ya Nduku.

“Alipoumwa alipewa dawa ya kutuliza maumivu na matroni wa shule, hakuwa katika hali mbaya, siku iliyofuata asubuhi wakati wa maandalizi hali yake ilizidi kuwa mbaya, akarudishwa kwa matroni bwenini, nikaonywa nikaenda kumuona, nilihisi hayuko vizuri, hivyo tukapanga njia ya haraka ya kumpeleka Machakos, kwa bahati mbaya alipelekwa Hospitali ya Level 5. darasani, ndipo tulipopigia simu familia kwa sababu alikuwa ametupa nambari ya nyanya yake,” alisema Ben Masila, mkuu wa shule.

Polisi wameanzisha uchunguzi wa kina huku familia hiyo ikisubiri matokeo ya uchunguzi wa maiti ili kubaini chanzo cha kifo cha ghafla cha Nduku.

machakos
Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka Machakos Consolata Nduku. Picha: Citizen TV Kenya.
Source: Youtube

Mwanafunzi wa kidato cha tatu aanguka na kufariki Kisii

Katika kisa kingine, familia moja katika kaunti ya Kisii iligubikwa na huzuni baada ya jamaa yao kuzirai na kufariki akiwa shuleni.

Mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu ambaye alikuwa mtoto wa kiume pekee katika familia yake, alikimbizwa katika hospitali ya Kisii Teaching and Referral Hospital, ambapo alitangazwa kufariki.

Pia soma

Magazetini: Serikali Yamsaka Jamaa wa Urusi Anayewarekodi Wanawake

Familia yake ilihitaji majibu huku wakihangaika kukubaliana na habari hiyo mbaya ya kifo chake cha ghafla.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *