Licha ya historia mbaya ambayo imekuwa nayo dhidi ya Simba, Dodoma Jiji FC imetamba kuwa haina hofu katika mechi baina ya timu hizo mbili kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kuanzia saa 1:00 usiku.

Katika mechi 10 za Ligi Kuu ambazo zimekutanisha timu hizo, Simba imepata ushindi zote ikifunga mabao 18 huku Dodoma Jiji ikifunga mabao mawili tu.

Hata hivyo pamoja na historia hiyo isiyo ya kuvutia, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Amani Josiah ametamba kuwa hawaiogopi Simba.

“Maandalizi kwenye kiwanja cha mazoezi yamekwenda vizuri kwa maana ya mambo ya kimbinu, mambo ya kiufundi lakini pia mambo ya kisaikolojia tuko vizuri kwenye eneo hio huku tukiifurahia mechi inayofuata mbele yetu ambayo ni mechi yenye ukubwa wake.

“Maisha kila siku yanabadiika na yana watu wapya. Tupo hapa kubadii baadhi ya vitu ambavyo vilikuwepo na nafikiri timu ambavyo ilikuwa inacheza msimu jana ni tofauti na msimu huu. Lakini pia tuko hapa kwa ajili ya kuchagiza kuona kama timu inapata matokeo bora kuliko yale yaliyopita.

“Baadhi ya vitu vinaweza kuanza leo. Mimi ninachoweza kukizungumzia ni kwamba nadhani sisi tumetoka kwenye mazingira magumu sana kuliko hata mechi yenyewe ya Simba kwa hiyo kuna vitu vingi vya kuhofia hata mechi ya Simba kwa hiyo mechi iko hapa kufurahia kuliko kuihofia. Hizi ni mechi ambazo unamuomba Mungu uwe sehemu ya mechi hizo kama sehemu ya kihistoria,” amesema Josiah.

Wakati Josiah akitamba hivyo, Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker amesema kuwa wanaingia wakiipa heshima kubwa Dodoma Jiji.

“Tumejiandaa vizuri kwa ajii ya hii wiki ambayo tunacheza mechi kadhaa nje ya nyumbani. Tumeanza kuonyesha dalili nzuri za kuwa na muendelezo mzuri wa kushinda mechi. Jambo la muhimu kwetu ni kutoonyesha dalili za kuridhika. Tunafahamu kwamba kesho tutakuwa na mechi ngumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda mchezo.

“Mechi ya muhimu zaidi ni iliyo mbele yetu kwa hiyo kwangu mimi natakiwa kupanga kikosi imara kesho. Kila mpinzani ana changamoto zake na hata kesho tunazitegemea. Wametoka kupata ushindi katika mechi ziizopita hivyo tunapaswa kuongeza umakini,” amesema Barker.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *