Dar es Salaam. Little ride, ni jukwaa la usafirishaji lililojengwa barani Afrika, leo limethibitisha upya dhamira yake ya kuendelea kuwekeza na kuhudumia soko la Tanzania kufuatia kujiondoa kwa Uber nchini.

Kampuni imesema inaongeza kasi ya upanuzi wa shughuli zake ili kuhudumia vyema abiria na madereva kwa kuzingatia mfumo endelevu wa usafiri unaoendana na mazingira ya ndani ya nchi.

Little ride inaendelea kupanua huduma zake ili kukidhi mahitaji ya abiria na madereva nchini Tanzania, huku ikitarajia ongezeko la mahitaji ya huduma zake katika kipindi kijacho.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Little ride, Kamal Budhabatti, amesema kuwa tukio hilo ni fursa muhimu kwa majukwaa ya Kiafrika kuongoza maendeleo ya miundombinu ya kidijitali ya usafiri barani Afrika.

“Kujiondoa kwa Uber ni hatua muhimu katika mwelekeo wa sekta ya usafiri nchini Tanzania. Ni ukumbusho kwamba majukwaa ya kidijitali yanapaswa kuelewa kwa kina soko, kanuni, na uhalisia wa kiuchumi wa madereva nchini. Little ride imejengwa Afrika, kwa ajili ya Afrika, na tunaongeza juhudi zetu maradufu hapa Tanzania,” alisema Budhabatti.

Aliongeza kuwa madereva ni mhimili wa majukwaa ya usafiri, na mkazo wa Little ride ni kuhakikisha wanapata kipato endelevu, viwango vya makato vilivyo nafuu, pamoja na ushirikiano wa muda mrefu. “Ukuaji wa biashara lazima ugawanywe kwa haki katika mfumo mzima wa usafiri,” alisisitiza.

Mbali na kuboresha uzoefu wa abiria, Little ride inaangalia pia kutoa huduma nyingine ikiwemo usafirishaji wa mizigo (logistics), usafiri wa mashirika (corporate mobility), pamoja na huduma za kidijitali kwa biashara ndogo na za kati (SMEs).

Little ride ni mtoa huduma kinara barani Afrika wa suluhisho za usafiri wa kibiashara na teksi za makampuni, ikihudumia mashirika ya kimataifa, biashara za kikanda, pamoja na taasisi za serikali zinazohitaji huduma za usafiri zilizo na mifumo madhubuti, zinazozingatia sheria, na zinazoweza kupanuka kwa urahisi.

Kampuni imeendesha shughuli zake katika masoko mbalimbali barani Afrika na kushirikiana kwa karibu na wadhibiti, washirika wa kibiashara, pamoja na taasisi za kifedha ili kuhakikisha uendeshaji endelevu na unaozingatia kanuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *