Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema kuwa uwekezaji wa zaidi ya shilingi bilioni 700 uliofanywa na Kilombero Sugar Company Limited una mchango mkubwa katika kupunguza changamoto ya ajira nchini, hususan katika sekta nyeti za uhandisi na taaluma nyingine za kiufundi.
Prof. Mkumbo ametoa kauli hiyo leo Februari 24, alipofanya ziara katika Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro, na kutembelea kiwanda hicho cha sukari.
(Feed generated with FetchRSS)