Msigwa: Kimara tulieni, Serikali ipo kaziniMsigwa: Kimara tulieni, Serikali ipo kazini

DAR ES SALAAM: WAKAZI wa Kimara jijini Dar es Salaam wameombwa kuwa wavumilivu kufuatia changamoto ya usafiri inayoendelea kulikumba eneo hilo, wakati serikali ikiendelea na jitihada za kutafuta suluhisho la haraka.

Ombi hilo limetolewa leo Februari 26, 2026 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini humo.

Msigwa amesema kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho za kusaini makubaliano na mzabuni wa Mofat ili kumuongezea muda wa kutoa huduma ya usafiri kati ya Kimara na katikati ya jiji, hatua inayolenga kupunguza adha kwa wakazi wa eneo hilo wakati wa mpito.

Aidha, ameeleza kuwa kampuni ya Trans Dar inatarajiwa kuanza kutoa huduma ya usafiri katika eneo la Kimara ikiwa na takribani mabasi 120 yenye viyoyozi (AC).

Kwa mujibu wa Msigwa, kuanza kwa huduma hiyo kunatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya usafiri na kuboresha huduma kwa wakazi wa Kimara na maeneo ya jirani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *