Alireza Arafi, mjumbe wa Baraza la Walinzi, ameteuliwa kuwa mjumbe halali wa Kamati ya Uongozi ya Iran, kuhudumu kama Kiongozi Mkuu hadi uchaguzi wa kiongozi mpya.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Arireza Arafi atakuwa sehemu ya Kamati ya Uongozi ya muda pamoja na rais Masoud Pezeshkian na Rais wa Mahakama Kuu Gholamhossein Mohseni Ejei.

Wakati huo huo Hezbollah imeapoa kuwa “itakabiliana na uchokozi” wa Marekani na Israel ambao umegharimu maisha ya Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei, Naim Qassem, mkuu wa kundi la Lebanon linalounga mkono Iran, amesema katika taarifa siku ya Jumapili.

“Tutatimiza wajibu wetu kwa kukabiliana na uchokozi,” kiongozi huyo wa Hezbollah amesema katika taarifa, akiongeza: “Chochote kitakachotolewa, hatutaacha njia ya upinzani.” Hezbollah haijaingilia kati tangu kuanza kwa mashambulizi makubwa kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran siku ya Jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *