Hii hudhihirika pale mathalani kesi ya ubakaji inaposhindikana kufika mahakamani, mwanamke anapokosa usaidizi katika kituo cha polisi, au anaponyimwa haki ya kulipwa kiwango sawa na mwanaume, urithi wa mali, na umiliki wa ardhi, jambo linalofanya iwe vigumu kwao kujenga maisha ya baadaye.

Mwanamke akishiriki katika maandamano ya kupinga ukatili wa kijinsia huko Quito, Ecuador.

© UN Women/Johis Alarcón

Mwanamke akishiriki katika maandamano ya kupinga ukatili wa kijinsia huko Quito, Ecuador.

Kwa nini wahalifu hawachukuliwi hatua?

Hali ya wahalifu kutoadhibiwa, ipo pale ambapo mwanamke anafanyiwa kitendo kinachomsababishia madhara, kisha hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtendaji. Hata sheria zikiwepo, hazitoi haki stahiki zenyewe bila msukumo kutoka nje.

Sheria kandamizi: Katika kila kona ya dunia, sheria bado zinawatendea wanawake na wanaume tofauti. Wanawake wana haki chache kisheria, jambo linaloamua nani wa kulindwa na nani wa kuaminiwa.

Vizuizi vya haki: Wanawake wanakumbana na hofu ya kulipiziwa kisasi, shinikizo la kukaa kimya kutoka kwa familia, gharama kubwa za mawakili, na mifumo migumu ya taasisi (polisi, mahakama, afya) ambazo hazifanyi kazi kwenye mfumo mmoja.

Mifumo ya Jamii: Mara nyingi tunawaza mashtaka yafikishwe katika mahakama za jinai, lakini dhuluma kubwa hutokea kwenye mifumo ya kijamii na utawala kama sheria za familia, migogoro ya kazi, nyumba, ardhi na uhamiaji.

Mashuhuda: kauli za watetezi na wahanga

Hizi ni kauli muhimu kutoka kwa wadau walio mstari wa mbele.

Matcha Phorn-In, Mtetezi wa wanawake nchini Thailand. 

“Kama huonekani katika maisha ya kila siku, mahitaji yako hayatafikiriwa. Sembuse kushughulikiwa, wakati wa mgogoro!”

Tony Mwebia, Mkurugenzi wa ‘Men End FGM’ nchini Kenya

“Huwezi kutumia ukamataji pekee kukomesha ukeketaji (FGM). Ikiwa misukumo na imani za kijamii zitabaki, familia zitatafuta njia za kukwepa sheria.”

Catherine Mootian, mtetezi wa AfyaAFRIKA, anazungumza kwa shauku juu ya ufahamu wa ukataji wa uzazi wa kike barani Afrika.

Catherine Mootian Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa AfyAFRIKA

Catherine Mootian, Mwathirika wa FGM, Kenya anasema, “wahalifu wanapofikishwa mahakamani, ni jambo muhimu. Lakini nini kinatokea kwa msichana aliyekeketwa? Nani anaunga mkono kupona kwake na elimu yake?”

Ljubica Fuentes, Mwanzilishi wa ‘Ciudadanas del Mundo’, nchini Ecuador.

“Hakuna sheria zinazozungumzia ukatili wa kidijitali. Ukienda kwa mtetezi wa umma, watakuambia usubiri hadi miaka mitano ndio litashughulikiwa. Una uhakika unataka kulianzisha jambo hili?”

Grecia Tardío, Mwanaharakati nchini Bolivia

“Mamlaka mara nyingi hazichukui hatua kwa sababu zinafikiri kwamba ikiwa lilitokea mtandaoni, basi si jambo la kweli.”

media:entermedia_image:38dcd669-5b67-4abd-ac00-772679337626

Courtesy of State Department for Gender and Affirmative Action, Kenya

Watu wakishiriki katika sherehe za kutia saini matamko ya mabaraza ya wazee ya kukomesha mila ya ukeketajikatika mikoa ya Samburu na Mlima Elgon nchini Kenya.

Mifumo ina kwama wapi?

Mifumo ya haki mara nyingi huonesha ukosefu uleule wa usawa uliopo kwenye jamii. Aliyetendewa ukatili au unyanyasaji anaweza kuhojiwa kwa umakini zaidi kuliko mhalifu, na jaji anaweza kuchunguza tabia na mavazi ya mwanamke badala ya kuangalia ridhaa ya kufanyiwa kitendo cha ngono.

Mifano ya Kimataifa: Chini ya utawala wa Taliban nchini Afghanistan, wanawake wameondolewa kabisa mahakamani na kwenye maisha ya umma. Nchini Sudan, ukatili wa kingono unatumika kama silaha ya vita huku kukiwa na ukosefu wa adhabu wakati mifumo ya sheria ikivunjika kutokana na machafuko. 

Nguvu ya Marekebisho: Marekebisho ya sheria za ndoa na familia tangu 1970 yamewawezesha zaidi ya wanawake milioni 600 kupata fursa za kiuchumi kwa kuimarisha haki zao za ndoa, mali, na urithi. Hii imewasaidia kuondoka kwenye mazingira ya ukatili na kujenga maisha mapya.

Vijana wakiandamana kupigania usawa wa kijinsia na haki za wanawake huko Nepal.

UN Women/Uma Bista

Vijana wakiandamana kupigania usawa wa kijinsia na haki za wanawake huko Nepal.

Haki ya kweli inapaswa kufananaje?

Ili mifumo ya haki iweze kuwatumikia wanawake na wasichana wote, inapaswa kuwa na:

Sheria zinazolinda walinda: Sheria zinazofafanua ridhaa ya ngono na kulinda waathirika, zilizoundwa kwa kushirikisha mashirika ya haki za wanawake.

Msaada wa kisheria unaofikika: Uwepo wa washauri wa kisheria wa jamii ili wanawake waweze kudai mishahara, mali, na ulinzi kwa vitendo.

Ufadhili wa kudumu: Mashirika ya haki za wanawake yanahitaji fedha za uhakika ili yaendelee kushinikiza mabadiliko, kwani mengi yanakaribia kufungwa kwa ukosefu wa fedha.

Uamuzi na takwimu: Kukusanya takwimu zinazoonesha mapengo ya kijinsia ili kuweza kufuatilia maendeleo na kuzuia juhudi kurudi nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *