SHINYANGA: Vikundi viwili vya wanawake halmashauri za wilaya ya Ushetu na Shinyanga vimekabidhiwa hundi yenye zaidi ya Sh bilioni 1.6 kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya kujiwezesha kiuchumi.

Hundi hizo zilikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo kimkoa yalifanyika kata ya Uyogo Halmshauri ya Ushetu.

Mhita alisema kuwezeshwa wanawake kiuchumi kumetokana na juhudi zilizofanyika kwenye kipindi cha awamu ya sita cha uongozi wa Rais Samia Suluhu kufanya mabadiliko ya sheria ili kuweza kunyanyua mwanamke kwenye nyanja mbalimbali za kiuchumi,kijamii na kibiashara.

“Kulingana na kauli mbiu ya haki kwa wanawake na wasichana ;msingi wa maendeleo jumuishi kufikia dira 2050 na sasa nimejionea harakati za kuinuka kiuchumi na kushiriki katika majukwaa na mabaraza ya kutoa maamuzi,”alisema Mhita.

Mhita alisema kupitia mapato ya ndani kwenye halmashauri wataendelea kutenga fedha na kutoa mikopo kwenye makundi ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Ofisa Maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga, Rehema Edson kabla ya vikundi hivyo kukabidhiwa hundi amesema halmashauri ya Ushetu kikundi kimoja cha wanawake kitapokea hundi ya zaidi ya Sh bilioni 1.4 na halmashauri ya Shinyanga itapokea hundi ya zaidi ya Sh milioni 233.6.

Edson amesema majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi yaliyokuwa yamefifia yamefufuliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu, Hadija Kabojela ametoa Sh 500,000 kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya jukwaa hilo.

Katibu wa jukwaa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Halmashauri ya Ushetu Hadija Jumanne amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa elimu ya ujasiriamali, mila potofu dhidi ya mwanamke katika umiliki wa mali na ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *