KATAVI: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande amewataka w
Watanzania kushirikiana na taasisi za uhifadhi nchini katika uhifadhi wa misitu kuongeza chachu ya maendeleo endelevu kupitia misitu iliyopo hapa nchini.

Kauli hiyo inakuja wakati Tanzania ikijiandaa kuadhimisha Siku ya Misitu Duniani.

Chande amebainisha hayo Mkoani Katavi katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba katika maeneo tofauti.

”Endeleeni kushirikiana na taasisi zetu za uhifadhi, Ili kusudi tubaki na maendeleo endelevu hasahasa katika maswala ya kilimo, kwa sababu bila ya misitu hakuna chakula, bila mvua hakuna chakula kwa hiyo ni muhimu sana kuhifadhi misitu yetu kwa kushirikiana,”amesisitiza Chande.

Akizungumza juu ya uhifadhi misitu ya jamii na manufaa yake, Chande ameahidi kuwa wizara itaendelea kushirikiana kwa karibu na jamii na viongozi kubainisha mipaka ya maeneo ya hifadhi za misitu na misitu ya jamii ili kuishi kwa mapenzi na utu kati ya wizara, taasisi na wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *