Kufuatia uamuzi wa Bodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) wa kuivua timu ya taifa ya Senegal, Lions of Teranga, Ubingwa wa AFCON 2025 na kuipa ubingwa huo timu ya taifa ya Morocco, serikali ya Senegal imeomba leo Jumatano uchunguzi wa kimataifa “kuhusu tuhuma za ufisadi ndani ya vyombo vya uongozi vya CAF.” Dakar imelaani uamuzi huo katika taarifa kuwa “haramu na usio wa haki” na kuahidi jibu kwa pande zote: michezo, kisheria, na kisiasa.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Senegal imeamua kupaza sauti. Serikali ya Senegal kupitia Marie Rose Khady Fatou Faye, Waziri na msemaji wake, imesema kwamba “bila shaka inakataa jaribio hili lisilo la haki la kuvuliwa ubingwa,” miezi miwili baada ya fainali ya iliyokuymbwa vurugu, ambapo Senegal ilishinda 1-0 katika muda wa ziada huko Rabat. Taarifa rasmi inabainisha “mshtuko mkubwa” wa mamlaka katika uamuzi ulioelezewa kama “tafsiri potofu ya wazi ya kanuni” na “kinyume na maadili ya michezo.”

Kulingana na Dakar, ubingwa huo “ulipatikana uwanjani, kwa mujibu wa sheria za mchezo,” na kubadilishwa kwake kunadhoofisha “matokeo ya kweli yaliyoshuhudiwa uwanjani.”

Serikali yatangaza mkakati wa majibu makubwa: ombi la “uchunguzi huru” kuhusu “tuhuma za ufisadi ndani ya CAF” na rufaa kwa “vyombo vyote vyenye uwezo, ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS),” ili “kurejesha ubora wa matokeo ya michezo.”

Taarifa hiyo inabainisha mshikamano wa Serikali na raia wa Senegal waliokamatwa nchini Morocco kufuatia matukio mabaya wakati wa mchezo wa fainali, na inaahidi “uhamasishaji kamili” kwa matokeo mazuri. “Senegal itaendelea kuwa imara, macho, na bila kutetereka katika kutetea haki za timu ya taifa na kurejesha heshima ya michezo ya Afrika,” msemaji huyo amebainisha.

Jumanne hii, Machi 17, Kamati ya Rufaa ya CAF iliivua Senegal, mshindi uwanjani, taji na kuitangaza Morocco kuwa bingwa wa Afrika bila kukusudia. Shirikisho hilo linahalalisha mabadiliko haya kutokana na tabia ya wachezaji wa Senegal, ambao waliondoka uwanjani kwa dakika kadhaa kufuatia uamuzi wa marefa katika muda wa ziada.

Katika ulimwengu wa soka la Afrika, uamuzi huo umesababisha mshtuko mkubwa miongoni mwa wapenzi wa soka. Kocha wa Ufaransa Claude Le Roy, kocha maarufu barani Afrika, ameekezea “kushtushwa” kwake na “maamuzi ya kipuuzi ya watu wasio na uwezo wanaoendesha soka la Afrika.” Amelaani uamuzi “uliochukuliwa ghafla, ambao hakuna mtu anayeweza kufiiria kilichotokea, uamuzi ambao ulichukuliwa bila kufikiria,” na akasema kwamba Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) “itabatilisha uamuzi huu na, bila shaka, kutambua ubingwa na ushindi wa Senegal.” Kwake, “hakuna mtu anayeweza kufikiria Senegal kukosa kurejeshwa ubingwa wake barani Afrika,” kwani uhalali wa kimchezo wa Simba wa Teranga, walioshinda uwanjani, hauna shaka machoni pake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *