Pakistan imetangaza kusitisha mapigano katika mzozo wake na Afghanistan leo Jumatano, Machi 18, wakati wote wa Sikukuu ya Eid al-Fitr, ambayo inaashiria mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari wa Pakistan amesema kwamba usitishaji huu wa mapigano, ambao utadumu kuanzia siku ya Alhamisi Machi 19 hadi siku ya Jumatatu usiku wa manane saa za ndani, unakuja “kwa ombi la nchi rafiki za Kiislamu, yaani Saudi Arabia, Qatar, na Uturuki.”

“Pakistan inatoa ishara hii ya nia njema kulingana na kanuni za Kiislamu,” waziri huyo amesema, “lakini katika tukio la shambulio la mpakani au ndege zisizo na rubani, au tukio lingine lolote la kigaidi,” operesheni ya kijeshi “itaanza tena kwa nguvu mpya.”

Uamuzi wa Islamabad unakuja siku chache baada ya shambulio la anga huko Kabul ambalo liliua mamia katika kituo cha matibabu ya dawa za kulevya, shambulio baya zaidi tangu mzozo kati ya nchi hizo mbili jirani uanze. Pakistan inashutumu mamlaka ya Taliban nchini Afghanistan kwa kuwahifadhi wapiganaji kutoka Taliban wa Pakistan (TTP), ambao wamedai kuhusika na mashambulizi mabaya katika ardhi ya Pakistan, shutuma ambayo serikali ya Afghanistan inakanusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *