
Watu wasiopungua wanane wamekufa na wengine kumi na saba wameokolewa wakati wa ajali ya Boti iliyokuwa ikisafirisha abiria na mizigo kadhaa ilipozama katika Ziwa Albert, baada ya kukabiliwa na upepo mkali, yapata saa mbili kutoka mahali pake eneo la Tchomia, mkowani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wawakilishi wa asasi za kiraia za eneo hilo Wanasema Mkasa huo ulitokea siku ya Jumatano usiku, katika Ziwa hilo Albert, karibu na kijiji cha Kamutasi, eneo la Djugu, mkoa wa Ituri, na kwamba hadi kufikia jana siku ya alhamisi watu kumi na saba pekee ndio waliokolewa wakiwa hai, na kwamba miili ya watu wanane ilipatikana na makumi yaw engine hawajulikani walipo.
Vyanzo hivyo vimesema jana kwamba manusura wa jail hiyo wameendelea kupewa matibabu katika vituo vya afya huko Angumu (mkoa wa Mahagi) na Linga (mkoa wa Djugu).
Maafisa wa idara ya usafiri wa majini wanasema ajali hiyo ilisababishwa na upepo mkali, lakini pia na kutokuwepo kwa hatua za kiusalama wakati wa upakiaji wa Boti, ikiwa ni pamoja na kuvaa jaketi za kuokoa maisha.
Kamishna wa Ziwa Albert, ambaye kwa sasa anaendelea na uchunguzi wa kina wa ajali hiyo, ameahidi kutoa ufafanuzi Zaidi kuhusu hali halisi ya ajali ya meli na kutangaza hatua za kuzuia majanga ya siku zijazo.