Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella, amefturisha waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu waliopo katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani na Kwaresima.
Akizungumza katika tukio hilo, amesema lengo kuu la futari hiyo ni kuimarisha umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa bila kujali tofauti za kidini huku akisisitiza umuhimu wa jamii kuendelea kudumisha amani na upendo.
Futari hiyo iliambatana na dua maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, pamoja na kuiombea nchi ili iendelee kuwa na amani, utulivu na mshikamano.
@deilahmomo
(Feed generated with FetchRSS)