Gazeti la Wall Street Journal limeripoti mapema leo Alkhamisi likiwanukuu maafisa wa serikali ya Marekani, kwamba Rais Donald Trump anahaha kutafuta njia ya kukomesha vita na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Vyanzo hivyo, ambavyo havikutajwa waziwazi, vimeiambia Wall Street Journal kwamba: “Trump amewataarifu wale walio karibu naye kwamba anataka kuepuka vita vya muda mrefu nchini Iran.”

Ripoti hiyo inasema: “Trump amewaambia washauri wake kwamba anaamini mzozo nchini Iran unaingia katika hatua zake za mwisho na kwamba wanapaswa kuzingatia ratiba iliyowekwa kwa Iran, ambayo ni wiki nne hadi sita za vita.”

“Trump anaogopa kuongezeka idadi ya vifo vya Wamarekani ikiwa vita na Iran vitaendelea,” limeripoti gazeti la Wall Street Journal likiwanukuu maafisa wa serikali ya Marekani.

Vyanzo hivyo pia vimeongeza kuwa Ikulu ya White House imepanga mkutano kati ya Trump na rais wa China katikati ya mwezi Mei, suala ambalo linaimarisha utabiri kwamba vita vya kiongozi huyo dhidi ya Iran vinaelekea kumalizika.

Ni vyema kusema hapa kuwa japokuwa Marekani na Israel zinaficha sana idadi halisi ya wanajeshi wa tawala hizo mbili walioangamizwa katika majibu ya Iran, lakini duru za kujitegemea zinasema mamia wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika vita vya sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *