Vita vya Mashariki ya Kati vimeingia mwezi wake wa pili leo Jumamosi, Machi 28, 2026, bila dalili zozote za kupungua, huku Israel na Iran zikiendelea kushambuliana kwa mabomu. Angalau waandishi wa habari wanne wa Lebanon wameuawa leo Jumamosi katika shambulio la anga la Israel kwenye gari lao kusini mwa Lebanon, waajiri wao wametangaza, wakithibitisha taarifa kutoka kwa chanzo cha kijeshi. Mauaji hayo yamesababisha ghadhabu nchini Lebanon.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kuuawa kwa waandishi wa habari wa Lebanon katika shambulio la anga la Israel kumesababisha ghadhabu nchini humo. Ali Shoueib, 55, alikuwa mwandishi nyota wa vita wa Al-Manar, kituo cha televisheni cha Hezbollah. Aliripoti kila mgogoro na Israel kwa zaidi ya miaka 30. Fatima Ftouni, katika miaka yake ya thelathini, alikuwa mwandishi wa habari wa kituo cha habari cha Kiarabu cha al-Mayadeen, ambayo safu yake ya uhariri iko karibu na Iran na Hezbollah, anaripoti mwandishi wetu huko Beirut, Paul Khalifeh.

Mbali na wanawake hao wawili, shambulio la anga, lililofanyika katika eneo la Jezzine, kilomita 25 kutoka mpakani na kilomita 20 kutoka mstari wa mbele, pia liliwaua wapiga picha wawili wa video waliokuwa ndani ya gari: mtoto wa Ali Choeib na kaka wa Fatima Ftouni.

Viongozi wa Lebanon, waliokosoa sana Hezbollah tangu mwanzo wa vita, kwa kauli moja wamelaani mauaji ya waandishi hao wa habari.

Mbali na Rais Joseph Aoun, ambaye amelaani “uhalifu mkubwa unaokiuka kanuni na mikataba yote ambayo waandishi wa habari wanastahili kulindwa kimataifa wakati wa vita,” Waziri Mkuu Nawaf Salam alilaani “ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu.”

kauli kama hiyo imepitishwa na Waziri wa Habari: Paul Morcos amesema kuwa shambuluo hilo “linalojirudi  na la kimakusudi” lililotekelezwa na Israel dhidi ya wanahabari  “halikubaliki” katika vita vya sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *