Serikali Wilayani Chamwino, imepiga marufuku kwa wananchi wanaofanya shuguli za kilimo na ufugaji kwenye vilima vinavyozunguka wilaya hiyo, kuondoka kwenye maeneo hayo, ili kuepusha mafurukio na mmomonyoko wa aridhi.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo ya Chamwino Bi. JANET MAYANJA, wakati alipokuwa akiendesha zoezi la upandaji wa miti 1,500 katika Ofisi ya Shirika la Umeme (TANESCO).

Naye, Meneja wa Tanesco Wilaya ya Chamwino Mhandisi JUDITH LIHAWA akaweka wazi ni kwanini Tanesco wamesukumwa kupanda miti, ambapo shilingi milioni 17 zimetengwa, huku mwakilishi wa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Dodoma Bw. JAMES VESO akiuhakikishia umma kuwa zoezi hilo ni endelevu.

#kilichoborakabisa

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *