Zaidi ya wanafunzi wa kitanzania 18 wamepelekwa nchini korea kwa ajili ya masomo ikiwa ni matokeo ya uhusiano mzuri baina ya tanzania na korea ambao umedumu kwa miaka mingi
Wakizungumza jijini Dar es salaam katika chuo cha United African University Of Tanzania (UAUT)mradi wa elimu ambao ni matokeo ya uwekezaji wa nchi ya korea makamu Mkuu wa Chuo cha United Africa University of Tanzania (UAUT) Sungsoo Kim pamoja na Profesa Thiery Noudui makamu msaidizi wa Chuo Kikuu cha United Africa University of Tanzania wamesema hatua ya kuwapeleka watanzania katika vyuo vya Korea ni sehemu ya mpango wa Chuo hicho katika kusaidia elimu kwa vijana na wanafunzi wa kila hali ili waje kusaidia taifa la tanzania .
Kwa upande wake sifa Yohana Masinga mlezi wa wanafunzi chuo cha united africa university of tanzania amesema nje ya scholarship pia chuo hicho kimeendelean kushirikiana na jamii ya watanzania ili kudumisha ushirikiano pamoja na maendeleo ya wanakigamboni
Nao baadhi ya wanafunzi Thomas Mazengo na Godson Charles walionufaika na nafasi za masomo nje ya nchi wamesema nafasi hizo zimelwta mabadiliko ya kielimu na kutwngeneza uwezo wa wao kushirilo katika kujenga taifa la tanzania .
(Feed generated with FetchRSS)