Waombolezaji nchini Israeli siku ya Jumatatu (Machi 30) walishiriki kwenye mazishi ya mwanajeshi wa IDF aliyeuawa katika shambulio la wapiganaji wa Hezbollah kutoka nchini Lebanon. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Sergenti Liran Ben Zion, mwenye umri wa miaka 19, aliuawa kwenye mapigano Kusini mwa Lebanon.

Lebanon iliingia kwenye mzozo unaoendelea mashariki ya kati Machi 2 baada ya wapiganaji wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran kurusha makombora kuelekea Israeli.

Wapiganaji wa Hezbollah walirusha makombora nchini Israeli kulaani mauaji ya kiongozi wa juu wa Iran Ali Khamanei.
Wapiganaji wa Hezbollah walirusha makombora nchini Israeli kulaani mauaji ya kiongozi wa juu wa Iran Ali Khamanei. REUTERS – Ronen Zvulun

Hezbollah walisema walichukua hatua ya kuishambulia Israeli kujibu mauaji ya kiongozi wa kiroho wa Iran Ali Khamanei aliyeuawa katika mashambulio ya Israeli na Marekani.

Tangu wakati huo, Israeli imewaagiza wakaazi wa kusini mwa Lebanon kuondoka, ikitekeleza mashambulio na oparesheni kwenye eneo hilo katika kile inasema ni juhudi zake na kupambana na wapiganaji wa Hezbollah.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *