
Mfululizo wa milipuko mikubwa ilisikika kusini mwa jiji la Bujumbura, mji wa kibiashara wa Burundi katika ghala la risasi kwenye kambi ya kijeshi ya Musaga.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Milipuko hiyo ilisababisha hofu na ajali kadhaa za magari katika vitongoji vya kusini karibu na eneo lililoathiriwa. Wakazi wengi walikimbia makazi yao, wakihofia huenda ni mapinduzi.
Hofu iliendelea kutanda kwa wakaazi wa jiji la Bujumbura kabla ya msemaji wa jeshi la Burundi Jenerali Gaspard Baratuza kujitokeza kwanza kupitia mitandao ya kijamii kuutuliza umma, akisema kwamba milipuko hiyo ilisababishwa na “ajali kubwa ya umeme” katika ghala la risasi.
“Jioni hii kumetokea ajali ya umeme katika kambi ya kijeshi ya Musaga, kuliko na ghala la silaha ambako umeme umesababisha ghala hilo kuteketea na kusababisha milipuko ya risasi na mabomu, ni hilo tu lililotokea usifkiri kuna kingine kimetokea ni kutuliza watu kwamba wahusika wanafanya kila jitihada ili kuepusha ajali kubwa zaidi. Watu watulize nyoyo, sio mashambulizi kama vile walivyokuwa wameanza kusema.”
Musaga ni miongoni mwa vitongoji vyenye watu wengi katika jiji la Bujumbura ambapo msemaji wa jeshi amewataka wakaazi wake na vitongoji jirani kusalia watulivu majumbani, ujumbe kama uo ukitolewa pia na wizara ya mambo ya ndani.
Burundi ni miongoni mwa nchi zilizowahi kushuhudia mapinduzi ya kijeshi katika miaka ya nyuma,inadaiwa kuwa kuna watu waliojeruhiwa katika kituo hilo la jana usiku.