Uwekezaji waimarika Tanzania robo ya kwanzaUwekezaji waimarika Tanzania robo ya kwanza

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma imetembelea kaya za watu wenye ulemavu wa macho kwa lengo la kutoa faraja, upendo na kuwajengea matumaini kuelekeza sikukuu za pasaka.

Ziara hiyo fupi imefanyika leo Aprili 2,2026 katika eneo la Matembebora wilayani Chamwino ikiongozwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Pendolake Elinisafi akiongozana na Meneja Msaidizi Huduma kwa Walipa Kodi, John Njau, pamoja na watumishi wengine.

Akizungumza katika ziara hiyo, Elinisafi amesema watu wenye ulemavu wa macho ni sehemu ya jamii inayothaminika, hivyo ziara hiyo imeacha ujumbe wa upendo na mshikamano, ikionesha dhamira ya TRA ya kuendelea kugusa maisha ya jamii sambamba na majukumu yake ya ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza kwa niaba ya wanakaya hao Mwenyekiti, Yeledi Cheleso ameishukuru TRA na ujumbe wake kwa moyo wa kujali na msaada walioutoa, akieleza kuwa hatua hiyo imeongeza faraja na kuwapa nguvu mpya ya kuendelea na maisha.

Kwa upande wake, Ofisa Maendeleo ya Jamii, Elizabeth ameipongeza TRA kwa kuendeleza mshikamano na jamii, akibainisha kuwa juhudi hizo zinaimarisha ushirikiano kati ya taasisi na wananchi, hususani kwa makundi yenye uhitaji maalumu.

Katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, TISEZA imepokea maombi 86 ya wawekezaji katika maeneo maalum ya kiuchumi (SEZ), ambapo kampuni 27 zimesaini mikataba ya uwekezaji. Miradi hiyo inatarajiwa kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 797.75 na kuzalisha ajira zaidi ya 20,460.

Sekta ya viwanda imeongoza kwa kuvutia uwekezaji kwa asilimia 51 ya miradi yote, huku pia ikiongoza kwa ajira na mtaji, ikifuatiwa na sekta za utalii, ujenzi, miundombinu na kilimo.

Kwa mujibu wa Teri, nchi za Asia zinaongoza kwa uwekezaji nchini, huku China ikichangia asilimia 39 ya uwekezaji na asilimia 60 ya ajira. Ndani ya nchi, mikoa ya Dar es Salaam na Pwani imeendelea kuwa vinara kutokana na miundombinu wezeshi.

Aidha, Watanzania wanamiliki zaidi ya asilimia 57 ya miradi yote ya uwekezaji, huku tofauti kati ya mtaji wa ndani na nje ikiwa ndogo, ambapo mtaji wa nje ni dola milioni 565 na wa ndani dola milioni 556.

Katika programu za EPZ na SEZ, miradi saba ilisajiliwa katika kipindi hicho, huku mtaji ukiongezeka kwa asilimia 51 hadi dola milioni 224.5 na mauzo ya nje kufikia dola milioni 752.2.

TISEZA pia imeendelea na kampeni za kuhamasisha uwekezaji wa ndani na kuanzisha vituo vya uwekezaji katika mikoa mbalimbali, pamoja na kuzindua kituo cha kusaidia vijana kupata masoko, mitaji na teknolojia.

Teri amesema mamlaka itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuimarisha huduma, kunadi fursa za uwekezaji na kushirikiana na sekta binafsi ili kukuza uchumi wa viwanda nchini.

Mwisho, amewataka watanzania kulinda mazingira ya uwekezaji kwa kudumisha amani, utulivu na mifumo imara ya kiuchumi, akisisitiza kuwa uwekezaji una mchango mkubwa katika kuongeza ajira, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *