Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amesema Serikali itaendelea kupeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maji katika Mji wa Kayanga wilayani Karagwe mkoani Kagera, kulingana na hati za madai zinavyowasilishwa.
Akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa Mhandisi Kundo ameeleza kuwa Serikali kwa sasa inatekeleza miradi miwili ya maji katika eneo hilo kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.
Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa Miji 28 wa Rwakajunju unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 64.3, pamoja na mradi wa usambazaji maji katika Mji wa Kayanga wenye thamani ya shilingi bilioni 1.31.
Mhandisi Kundo amesema kuwa kwa pamoja miradi hiyo imefikia wastani wa asilimia 70 ya utekelezaji, na inatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 356,790 wanaoishi katika Mji wa Kayanga na maeneo ya jirani.
Aidha, amebainisha kuwa hadi kufikia mwezi Machi 2026, Serikali ilikuwa tayari imelipa jumla ya shilingi 42,981,808,276.08 kwa ajili ya kuendeleza utekelezaji wa miradi hiyo, huku akisisitiza dhamira ya Serikali kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
#kilichoborakabisa
(Feed generated with FetchRSS)