Nchi ya China inalenga kuongeza kasi ya ukarabati wa reli kati ya Zambia na Tanzania, kwa lengo la kuiwzesha taifa hilo la Asia kupata madini muhimu ya metali.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

China kwa sasa inaismarisha udhibiti katika njia zinazotumiwa Afrika katika usafirishaji wa madini ya shaba, ambapo kwa kufufliwa kwa reli ya kimakakati kati ya Zambia na Tanzania, Beijing inatafuta kudhibiti mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka kwenye mgodi hadi bandarini.

Mradi huu, wenye thamani ya zaidi ya Dola Bilioni Moja, uko katikati ya ushindani unaokua kati ya China na nchi za Magharibi kwa ajili ya upatikanaji wa metali muhimu.

Kwa sasa madini ya shaba yanayochimbwa barani Afrika husafirishwa na kampuni hadi kwenye meli za China, lakini sasa ukarabati wa reli ya Tazara, Beijing itafanikiwa kuzafirisha madini ya shaba kutoka nchini Zambia na DRC hadi kwenye bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania.

Katika hatua nyingine, Marekani na Umoja wa Ulaya nao pia wanaendelea na miradi yao ya reli ya Lobito, hatua inayoashiria wazi ushindani uliopo  katika kupata madini muhimu ya Afrika baina ya China na Marekani na ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *