Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Priscus Joseph amesema mabadiliko ya nauli hayapo mikononi mwa wamiliki wa mabasi bali hupangwa na mamlaka husika za serikali. Amesisitiza kuwa si halali kwa mmiliki wa basi kupandisha nauli kiholela kwa kisingizio cha kupanda kwa bei ya mafuta.
Ameeleza kuwa utaratibu uliopo unahitaji kufuatwa ili kulinda maslahi ya abiria na wadau wote wa sekta ya usafirishaji, na kwamba hatua zozote za kubadili nauli lazima zipitie mamlaka zinazohusika.
Aidha, amesema pale bei ya mafuta inapoongezeka na kuathiri gharama za uendeshaji, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hutoa mwongozo maalum ili kuhakikisha kunakuwa na uwiano unaozuia hasara kwa wamiliki wa mabasi pamoja na kulinda haki za abiria.
#AzamTVUpdates
Halima Abdallah
@goodluckpaul_mc
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)