
Nchi ya Rwanda inaendelea na kumbukizi ya miaka 32 ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994, ambapo watu zaidi ya laki 8 waliuawa wengi wao wakiwa ni Watusi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Raoul Shungu ni mkazi wa Kigali, anasema alipoteza ndugu zake wakati wa mauaji ya kimbari.
“Wakati wa mauaji ya kimbari tarehe 7 Aprili, nilikuwa bado sijazaliwa, ilikuwa ikisalia mwezi mmoja tu nizaliwe, kwani nilizaliwa tarehe 10 Mei mwaka huo. Mama yangu alikuwa na ujauzito wa miezi minane.Ingawa mama yangu bado yuko hai, kati ya watoto 9 kutoka kwa wazazi wake, wote walifariki kutokana na mauaji ya kimbari, pamoja na wazazi wake wote wa upande wa mama na wa baba. Sina ndugu yoyote kutoka upande wa baba wala mama yangu.” alisema Raoul Shungu.
Romario Abdul Djabari Gakuba ni miongoni mwa manusura wa mauaji ya kimbari.
“Nimenusurika mauaji ya kimbari lakini pia nashukuru Mungu nimenusurika kutoka katika familia ya watu watano ambapo mimi peke yake ndio nimenusurika kwa sababu nilikuwa Uganda, nilikuwa nimeeda kusoma Uganda na kurudi nikapata familia yote imeuuawa.”
Wizara ya Umoja wa wanyarwanda (MINUBUMWE), imeeleza kuwa wiki hii ya maombolezo, bendera ya taifa itapeperushwa nusu mlingoti kwa muda wa siku 100.
Christopher Karenzi Kigali, RFI Kiswahili