Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dkt.Maimbo Mndolwa amesema Tume ya uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29 ni huru na wananchi wanamatumaini makubwa na Tume hiyo.
Dkt Mndolwa amesema hayo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari na kueleza kuwa ni busara kama taifa kushugulikia changamoto zake yenyewe kabla ya kuomba msaada kutoka nje ya nchi.
Katika hatua nyingine Askofu Dkt. Mndolwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Tume hiyo ili itafute kwanza suluhu ya ndani na Jambo hilo kuonesha dunia ukomavu wa Demokrasia na Siasa.
#kilichoborakabisa
(Feed generated with FetchRSS)