KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuhamasisha amani, umoja, mshikamano na maridhiano kwa manufaa ya taifa.
Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Idara ya Habari ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Msigwa amesema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kuathiri mwelekeo wa jamii, hivyo vinapaswa kutumika kwa uwajibikaji.

Ameeleza kuwa tasnia ya habari ina mchango mkubwa katika kuhamasisha maendeleo ya wananchi na kufanikisha malengo ya taifa, ikiwemo Dira ya Maendeleo 2050. Msigwa alibainisha kuwa serikali imefanya maboresho ya kisheria ili kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari, akimpongeza Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuboresha mazingira ya kazi kwa wanahabari.
Aidha, alionya kuwa matumizi mabaya ya vyombo vya habari yanaweza kusambaza taarifa za uchochezi na kuhatarisha amani ya nchi. SOMA: Wale ambao hawana Ithibati watupishe