Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Marekani Donald Trump anasema Marekani itaongeza muda wa kusitisha mapigano na Iran, kwa ombi la Pakistan, na kuendelea na vizuizi vya kijeshi katika bandari za Iran.
Tangazo la Donald Trump kwamba amekubali kuongeza muda wa kusitisha mapigano na Iran bila kikomo maalum ni mabadiliko makubwa ikilinganishwa na msimamo wake wa saa chache zilizopita.
Trump alisema kupitia mitandao ya kijamii “kwa kuzingatia kwamba serikali ya Iran imegawanyika sana, jambo ambalo halikutarajiwa kuwa tofauti, na kufuatia ombi la Field Marshal Asim Munir pamoja na Waziri Mkuu Shehbaz Sharif wa Pakistan, tumeombwa kusitisha shambulio letu dhidi ya nchi ya Iran hadi wakati ambapo viongozi wao na wawakilishi wao wataweza kuwasilisha pendekezo la pamoja”
Aliongeza; “kwa hiyo, nimeelekeza jeshi letu kuendelea na zuio, na katika mambo mengine yote, liendelee kuwa tayari kikamilifu. Hivyo basi, nitaongeza muda wa kusitisha mapigano hadi pendekezo lao litakapowasilishwa na mazungumzo kukamilika, kwa namna yoyote ile.”
Awali akizungumza na CNBC, Trump alisema “natarajia tutakuwa tunashambulia” na kwamba jeshi lilikuwa “tayari kabisa kuanza.” Aidha alirejea tishio lake la kuharibu madaraja yote na mitambo ya umeme nchini Iran.
Hata hivyo, saa chache kabla ya muda wa awali wa kusitisha mapigano kuisha, amekubali kusitisha mapigano kwa muda usio na kikomo. Katika kipindi chote cha mgogoro huu, Trump amejaribu kutumia vitisho dhidi ya serikali ya Iran kwa matamshi makali.
Sasa inaonekana dhahiri hataki kuanza tena kuhusu mashambulizi dhidi ya Iran.