Urusi imetangaza siku ya Jumanne, Aprili 21, kwamba iliwakomboa mateka wawili katika operesheni maalum nchini Mali. Raia hao wananaelezewa kuwa ni mmja kutoka Urusi na Muikraine mmoja, waliokuwa wanashikiliwa na wanajihadi tangu walipokamatwa katika nchi jirani ya Niger mnamo mwaka 2024.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwezi Agosti 2024, kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (GSIM), linaloshirikiana na Al-Qaeda, lilidai katika video isiyo na tarehe kuwashikilia “mateka wawili wa Urusi” ambao walisema walitekwa nyara kusini-magharibi mwa Niger kwa tarehe isiyojulikana.

“Vikosi vya wanamgambo wa Africa Corps, katika ardhi ya Jamhuri ya Mali, viliwaokoa wafanyakazi wa kampuni ya uchunguzi wa jiolojia ya Urusi wakati wa operesheni maalum. Walikamatwa mwezi Julai 2024 nchini Niger” na wanamgambo wa kundi la GSIM, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Kikosi cha Africa Corps ni kitengo kilio chini ya amri ya moja kwa moja ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi, ambacho kilichukua nafasi ya kundi la wanamgambo la Wagner barani Afrika. Katika taarifa ya wizara hiyo, wanaume hao wawili wanatambuliwa kama Oleg Greta, Mrusi aliyezaliwa mwaka wa 1962, na Yuri Yurov, raia wa Ukraine aliyezaliwa mwaka wa 1970. Hakuna ripoti za majeruhi kwa operesheni hiyo zilizotolewa.

Urusi mara chache hutoa maoni kuhusu shughuli zake za kijeshi katika Sahel, ambapo imeimarisha ushawishi wake kufuatia mfululizo wa mapinduzi dhidi ya Magharibi. Kutokana na majaribio ya Magharibi ya kuitenga kutokana na vita nchini Ukraine, Urusi imejaribu kuunda ushirikiano mpya barani Afrika, ambapo imepanua ufikiaji wake wa kisiasa, kiuchumi, na kijeshi katika miaka ya hivi karibuni.

Wanajeshi wa Urusi au wakufunzi wa kijeshi wameripotiwa kutumwa Mali, Niger, Burkina Faso, Equatorial Guinea, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Libya. Baadhi ya mataifa haya yamekuwa yakikabiliwa na vurugu za mara kwa mara na hatari za kijihadi kwa miaka mingi, zinazofanywa na makundi ya kijihadi yayohusiana na Al-Qaeda na Islamic State(ISIS).

Kulingana na Moscow, Kikosi cha Africa Corps kinachangia “vita dhidi ya ugaidi” na “kuimarisha utulivu wa kikanda” katika Sahel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *