
Kundi la kwanza la wakimbizi 470 wa DRC kutoka Burundi wamerudi katika jiji la Uvira (Kivu Kusini) siku ya Alhamisi, Aprili 23, kulingana na Shirika la Umoja w Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Burundi. Waliingia kupitia kivuko cha mpaka cha Kavimvira, ambapo walipokelewa na ujumbe kutoka serikalini na UNHCR.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Operesheni hii inakuja baada ya kusubiri kwa muda mrefu kwa wakimbizi hao, ambao walikuwa na hamu ya kurudi nyumbani.
Msafara huo uliondoka katika kambi ya Busuma katika mkoa wa Ruhigi siku ya Alhamisi asubuhi. Kuwasili kwao Uvira kulitarajiwa kati ya saa 9:30 alasiri na saa 10:00 alasiri (saa za Afrika ya Kati). Mwakilishi wa UNHCR nchini Burundi, Brigitte Eno, alielezea:
“Tunatoa usafiri kutoka Burundi.” Wakifika DRC, watu hawa watapokea kile tunachokiita “kifurushi kidogo cha mahitaji muhimu” ili kuwasaidia kuungana tena kwa usalama na kwa heshima na familia zao. Hii itatolewa na UNHCR na washirika wengine nchini DRC. Hasa, WFP pia itatoa mgao wa chakula wa miezi miwili, na UNHCR itatoa msaada wa pesa taslimu kwa watu wazima na watoto, pamoja na usaidizi wa kuingizwa tena kwa watoto katika mfumo wa elimu.
UNHCR yaandaa watakapofikia wakimbizi
Mara tu walipowasili DRC, watu hawa walipokelewa Kavimvira katika eneo lililoandaliwa na UNHCR. Kulingana na mwakilishi wa UNHCR huko Uvira, ushiriki wa mashirika ya kiraia ni muhimu kwa operesheni hiyo kuendelea vizuri.
Kwa upande wake, Naibu Gavana wa Kivu Kusini, Jean Jacques Elakano, amebainisha kwamba hatua zote muhimu zimechukuliwa ili kuhakikisha wakimbizi hao wanarudi kwa amani. Anahakikisha kwamba usalama umezingatiwa katika maeneo watapofikia.
Baada ya waasi wa AFC/M23 kuuteka mji wa Uvira, katika mkoa a Kivu Kusini, mapema mwezi Desemba 2025, kati ya Wakongo 60,000 na 65,000 walikimilia nchini Burundi ndani ya takriban siku kumi, kulingana na mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na UNHCR na IOM.