
Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila, ikimtuhumu kwa kuwaunga mkono waasi wa kundi lenye silaha la M23.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa zamani wa Kongo Joseph Kabila, ambaye aliongoza DRC kuanzia 2001 hadi 2019, sasa yupo kwenye orodha ya watu wanaolengwa na vikwazo vya kiuchumi kutoka kwa serikali ya Marekani.
Kulingana na Washington kiongozi huyo wa zamani analenga kuivuruga serikali ya DRC kwa kuunga mkono kundi la M23/ AFC.
Aidha imebainika kuwa Kabila aliishi chini ya ulinzi wa M23 mwaka jana huko Goma, ngome ya kundi hilo lenye silaha mashariki mwa nchi.