Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki Kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani Imedhamiria kuwatumia watanzania wanao ishi ughaibuni hususani nchini Ujerumani kama kete Muhimu ya kujenga uchumi wa hapa Tanzania ambapo takwimu zinaonesha kutoka mwaka 2024 hadi Mwezi julai mwaka 2025 jumla ya shilingi trilioni trilioni 4.9 zimetumwa nchini kutoka kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi.

Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano maalumu baina ya watanzania wanao ishi ughaibuni na Taasisi za umma na binafsi zilizo enda jijini Berlin nchin Ujerumani,Balozi wa tanzania Ujerumani Hassani Mwamweta amesema WATANZANIA wanao ishi ughaibuni kupitia Kongamano hilo watapata huduma Muhimu ambazo imekuwa vigumu kuzipata wakiwa Ujerumani ili kuwawezesha kufanya shughuli zao vizuri

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha Diaspora kutoka wizara ya mambo ya nje salvatory mbilinyi akatoa takwimu za fadha zilizo tumwa tanzania kwa shughuli mbali mbali huku akiendelea kuwaaasa watanzia kuendelea kuwa na uzalendo wa kuwaza nchi yao mahali popote walipo
Baadhi ya Taasisi zilizo shiriki katika Kongamano hilo nao wakaeleza umuhimu wa wao kuwa katika jukwaa hilo

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *