Wakulima wa Pamba kutoka Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, wameishukuru serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa usaidizi wake mkubwa katika sekta ya kilimo cha Pamba kwa kutoa mbegu, mbolea na viuatilifu vilivyosaidia kuimarisha na kukuza tija ya zao hilo kwa wakulima pamoja na kuongeza uchumi.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 07, 2026, wananchi hao wameishukuru pia serikali kwa kuongeza idadi ya Maafisa ugani katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo, suala ambalo limesaidia katika usaidizi wa kitaalamu, usimamizi na ushauri kwa wakulima na hivyo kusaidia katika kupunguza gharama za uzalishaji pamoja na kuongeza thamani ya zao hilo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *