Msemaji mkuu wa serikali na katibu mkuu wa wizara ya habari na mawasiliano Gerson Msigwa amesema kumekuwa na mfululizo wa uvujaji wa siri za serikali, jambo linalofanywa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu huku akitoangalizo kuwa serikali iko macho na wote wanaotekeleza vitendo hivyo watasakwa na kukamatwa.
Msigwa ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa habari na mawadiliano serikalini ambacho kinaendelea mkoani njombe, huku akiwatahadharisha maofisa habari hao kutokuwa sehemu ya wale wanaovujisha nyaraka za siri za serikali.
Kando na hilo msigwa amelalamikia kutukanwa katika mitandao ya kijamii huku akiwataka maafisa habari kutonyamaza, tahadhari zaidi ikielekezwa kwa wananchi kutojihusisha na kutoa lugha za matusi katika mitandao ya kijamii.
Ameongeza kuwa zaidi ya vijana 400 wamekamatwa kwa tuhuma za kutoa lugha za matusi katika mitandao ya kijamii.
Kikao cha maofisa habari, mawasiliano na itifaki kinaendelwa katika mkoa wa Njombe ambapo zaidi ya maafisa habark wa serikali 500 wamehudhuria kikao hicho kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
#Startvhabari
@dkhan1410
(Feed generated with FetchRSS)