Binti Moza Salum Nassoro mwenye umri wa miaka minane kutoka Kanyenye, Tabora, aliibua hisia na kuvutia mamia ya watu katika maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi yaliyofanyika kwenye viwanja vya FFU Tabora baada ya kusisitiza kuwa anatamani kuonana na Samia Suluhu Hassan, Akiwa na ujasiri mkubwa, alimfuata MC Baraka na kueleza ndoto yake ya siku moja kusalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jambo lililowafanya wengi kushangazwa na kujiamini kwake akiwa na umri mdogo.
Baada ya kuonyesha msisitizo mkubwa, viongozi walikubali ombi lake na jina lake likatangazwa rasmi mbele ya wageni. Alipopata nafasi ya kuzungumza, Moza alisema ndoto yake ni kuwa mwandishi wa habari.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika Mei 9, 2026, yalijumuisha gwaride, michezo mbalimbali na maonesho ya mbinu za kazi za polisi, yakilenga kuimarisha mshikamano kati ya askari, familia zao na wananchi.
@deilahmomo
(Feed generated with FetchRSS)