Mshauri wa ngazi ya juu wa Kiongozi Muadhamu: Uvumilivu haupo siku zote/ Azitahadharisha nchi za Kiarabu za Ghuba ya UajemiMshauri wa ngazi ya juu wa Kiongozi Muadhamu: Uvumilivu haupo siku zote/ Azitahadharisha nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi

Mshauri wa ngazi ya juu wa Kiongozi Muadhamu: Uvumilivu haupo siku zote/ Azitahadharisha nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi

Mohammad Mokhber ameandika katika akaunti yake ya X kwamba Iran kwa miaka sasa imekuwa ikiamiliana na nchi jirani za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi kama nchi rafiki na ndugu lakini nchi hizo zimechagua kushirikiana na maadui wa Iran na Palestina akiashiria wazi Marekani na utawala wa Israel.

Mshauri wa ngazi ya juu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kusema katika ujumbe wake huo aliouchapisha kwa lugha ya Kifarsi kwamba: “…kwa kuuza uhuru wao mapema, hata waliweka ardhi na nyumba zao mikononi mwa maadui wa Palestina na Iran,” akimaanisha Marekani na Israel.

Iran ilizishambulia kambi za kijeshi za Marekani katika nchi za Ghuba ya Uajemi kujibu uvamizi wa Marekani na Israel ulioanza mwishoni mwa mwezi Februari na kisha hujuma hiyo ya kijeshi ikasitishwa kufuatia usitishaji vita uliotangazwa mwezi Aprili mwaka huu.

Nchi hizo za Ghuba ya Uajemi hususan Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambayo yalishambuliwa pakubwa na Iran wakati wa uvamizi wa Marekani na Israel, zimeituhumu Iran kuwa ilikiuka mamlaka ya kujitawala nchi hizo huku zikijaribu kuiwekea mashinikizo Tehran kupitia njia za kidiplomasia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *