
Muigizaji maarufu wa Kihispania amesema kando ya Tamasha la Filamu la Cannes kwamba: Licha ya kampeni yake ya hadharani dhidi ya vita vya Israel na mauaji ya kimbari ya utawala huo huko Gaza, Palestina, anafanya kazi zaidi kuliko hapo awali, na hii ina maana ya kubadilika simulizi kuhusu vita vya Gaza.
Katika sherehe ya mwezi Februari ya Oscar, alipokuwa akikabidhi tuzo ya filamu bora ya kimataifa, nyota maarufu wa sinema, Javier Bardem alisema: “Hapana kwa vita” na “Palestina Ipewe Uhuru.”
Bardem, ambaye yuko kwenye Tamasha la Filamu la Cannes mwaka huu akiwa na filamu ya “The Beloved” iliyoongozwa na mkurugenzi wa Uhispania Rodrigo Soroguin, ameiambia AFP kwamba: “Licha ya kampeni yake ya hadharani dhidi ya vita vya Israel huko Gaza, anafanya kazi zaidi kuliko hapo awali, na hii ina maana ya kubadilika simulizi kuhusu vita vya Gaza. Nadhani ni muhimu kuweza kutoa maoni yako, ukijua kwamba kutakuwa na watu wanaokubaliana na watu wasiokubaliana nawe.”
Ameongeza: “Kwa kweli, ninawasiliana zaidi kuliko hapo awali kwa sababu simulizi inabadilika. Sasa tunaelewa kwamba unapounga mkono au kuhalalisha mauaji ya kimbari kama kile kinachotokea sasa, jambo hili huwa na matokeo, na jamii inajua hilo.”
Wasani na waigizaji wengi wa kimataifa wamekuwa wakipinga mauaji ya kimbari na unyama unaoendelea kufanywa na Israel- ikiungwa mkono na nchi za Magharibi- dhidi ya watu wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza.
